Team meeting
MAKUBALIANO YA MTUMIAJI (User Agreement)
1. Uhalali wa Matumizi
Lazima uwe mtu mzima (18+) na mfanyabiashara halali. Unawajibika kutuma ujumbe wa ukweli, bila kudanganya au kutapeli.
2. Sender ID
Lazima uthibitishe Sender ID kabla ya kuitumia. Usitumie jina la biashara au mtu mwingine bila idhini yake au ya mamlaka husika.
3. Ujumbe Haramu
Hairuhusiwi kutumia AkiliSMS kutuma:
- Ujumbe wa utapeli (fraud)
- Spam bila ridhaa ya mpokeaji
- Ujumbe wa matusi, kejeli, au kuharibu amani au maadili ya jamii
4. Kusimamishwa
Akaunti yako inaweza kusimamishwa au kufutwa ukikiuka makubaliano haya.
5. Uwajibikaji
AkiliSMS haitawajibika kwa hasara yoyote utakayopata kutokana na matumizi mabaya ya mfumo huu.
6. Sheria
Unakubali kufuata sheria za Tanzania pamoja na kanuni za TCRA.
7. Utoaji wa Taarifa kwa Mamlaka
Uongozi wa AkiliSMS una ruhusa ya kutoa taarifa zako kwa TCRA, mamlaka za serikali au vyombo vya dola endapo itathibitika umetuma SMS za utapeli au ukiukaji wa sheria kupitia mfumo wetu.

MASHARTI YA MATUMIZI (Terms & Conditions)
1. Usajili
Unatakiwa kutoa taarifa sahihi unaposajili akaunti kwenye AkiliSMS.
2. Majukumu Yako
Unawajibika kwa ujumbe wote unaotumwa kupitia akaunti yako.
3. Sender ID
Sender ID yoyote lazima ipitishwe na AkiliSMS kabla ya matumizi.
4. Matumizi Mabaya
Hairuhusiwi kutumia mfumo huu kwa utapeli, spam, au ujumbe wa uongo.
5. Ufuatiliaji
AkiliSMS inaweza kufuatilia matumizi ya mfumo ili kuzuia matumizi mabaya.
6. Kuwajibika
AkiliSMS haitalipa fidia ya hasara yoyote inayotokana na matumizi ya huduma zetu.
7. Mabadiliko ya Masharti
Tunayo haki ya kubadilisha masharti haya muda wowote, na utajulishwa kupitia mfumo wetu.
8. Utoaji wa Taarifa kwa Mamlaka
Uongozi wa AkiliSMS una ruhusa ya kutoa taarifa zako kwa mamlaka husika endapo itathibitika umetumia huduma yetu kinyume cha sheria.